- Tujifunza kufanya kichaa cha mbwa kuwa Historia
Kichaa cha mbwa ni nini?
- Kichaa cha mbwa ni ugonjwa unaosababishwa na Virusi ambavyo huwa kwenye mate ya mnyama mngonjwa.
- Virusi hivi husambazwa kwa binadamu na wanyama kupitia kuumwa/kung’atwa na mnyama aliyeambukizwa.
- Mara tu dalili za kichaa cha mbwa zinapoanza, matokeo yake huwa ni kifo.
Nini kinasababisha kichaa cha mbwa?
- Kichaa cha mbwa kinasababishwa na Virusi, vimelea ambao ni wadogo kuliko bacteria.
- Vimelea wa Kichaa cha mbwa wakiingia mwilini hushambulia na kuharibu mfumo kati wa fahamu
- Mfumo kati wa ufahamu unajumuisha Ubongo na uti wa Mgongo.
- Mfumo wa fahamu ulio na afya ni muhimu kwa; Kufikiri, Kuhisi, kuona, kupumua, kumeza, kula, kutembea na kuongea.
Wanyama gani wanapata kichaa cha mbwa?
Virusi vya kichaa cha mbwa vinaweza kumuingia mnyama yeyote aina ya mamalia.
- Wanyama kama vyura, Ndege na Nyoka hawawezi kupata kichaa cha mbwa
- Baadhi ya wanyama wanaoeneza kichaa cha mbwa ni, Mbwa, Popo, Mbweha na Paka
- Mbwa ndiye kisababishi kikuu cha kichaa cha mbwa kwa Binadamu Duniani kote
Mnyama mwenye kichaa cha mbwa ana dalili gani?
- Mbwa na paka wanapokuwa na kichaa cha mbwa huonyesha dalili kadhaa kama vile;
- Kuwa na uoga na kuchanganyikiwa
- “Kuogopa maji" na kushindwa kumeza kutokana na matatizo kwenye koo
- Kudondokwa na mate kwa wingi
- Wanyama wa mwitu wenye ugonjwa huu hubadili tabia zao kwa mfano, wanao onekana usiku peke yake huonekana wakizurura mchana.
- Mbwa, paka, farasi, ng’ombe, kondoo na mbuzi pia huonyesha dalili za unyonge, kujiumiza au kujing’ata vile vile kutoweza kustahimili mwangaza.
Nifanye nini ili kuzuia kichaa cha mbwa?
- Hakikisha wanyama wako wamechanjwa na afisa wa kudhibiti wanyama kuzuia kichaa cha mbwa
- Ita wataalamu wa wanyama ukiona mnyama mgonjwa
- Hakikisha kuwa sehemu za kutupia makombo na taka haziwavutii wanyama wa porini
- Mnyama wa kufugwa atakiwa kuangaliwa kwa muda wa siku kumi(10) kwa dalili za kichaa cha mbwa.
Nifanye nini mnyama wangu anapomuuma mtu?
- Mhimize mtu huyo akamwone daktari haraka iwezekanavyo.
- Mwone daktari wako wa mifugo kubaini kama chanjo ya mnyama wako iko sawa kulingana na wakati wake.
- Itabidi mnyama wako azuiliwe na aangaliwe kwa muda wa siku kumi (10) kwa dalili za kichaa cha mbwa.
- Piga ripoti kwa afisa wako punde tu utakapoona dalili za ugonjwa wa kichaa cha mbwa.
- Baada ya uchunguzi huu, hakikisha mnyama wako amepata chanjo dhidi ya kichaa cha mbwa.
Nifanye nini mnyama wangu anapoumwa?
- Mwone daktari wako wa mifugo ili mnyama huyo apate chanjo dhidi ya kichaa cha mbwa hata kama alikuwa keshachanjwa.
- Itabidi umzuilie mnyama wako na kumwangalia kwa muda wa siku arobaini na tano(45) ama zaidi kwa dalili za kichaa cha mbwa.
- Mbwa na paka ambao hawakuwa na chanjo itabidii wauwawe au wazuliwe kwa muda wamiezi sita (6).
- Wanyama wengine isipokuwa mbwa na paka, waking’atwa, itabidii wauwawe haraka iwezekanavyo
Nifanye nini ninapoumwa na mnyama?
- Usiwe na hofu! Safisha kidonda vizuri kwa kutumia maji mengi na sabuni
- Mwone daktari haraka iwezekanavyo kupata chanjo dhidi ya kichaa cha mbwa na ufuate maagizo yake.
- Wasiliana na afisa wa kudhibiti wanyama kuthibitisha kama mnyama alikuwa amechanjwa.
- Ikiwezekana, mzuilie ama mnase mnyama wa kufugwa ili aweze kuangaliwa kwa muda wa siku kumi(10) kwa dalili za kichaa cha mbwa.
- Ikiwa ni mnyama wa pori, jaribu kumnasa ikiwezekana. La sivyo itabidi auwawe bila kuharibu sehemu ya ubongo kwani utahitajika kuchunguzwa kama alikuwa na kichaa cha mbwa.
- Matibabu yanayofanyika kwa wakati mwafaka baada ya kuumwa yaweza kuzuia mtu kuambukizwa na kichaa cha mbwa.
Taarifa hii imeletwa kweni na;
KENYA WOMEN VETERINARY ASSOCIATION
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.