Monday, September 5, 2011

WORKING TOGETHER TO MAKE RABIES HISTORY

  • Tujifunza kufanya kichaa cha mbwa kuwa Historia


Kichaa cha mbwa ni nini?
  • Kichaa cha mbwa ni ugonjwa unaosababishwa na Virusi ambavyo huwa kwenye mate ya mnyama mngonjwa.
  • Virusi hivi husambazwa kwa binadamu na wanyama kupitia kuumwa/kung’atwa na mnyama aliyeambukizwa.
  • Mara tu dalili za kichaa cha mbwa zinapoanza, matokeo yake huwa ni kifo.



Nini kinasababisha kichaa cha mbwa?

  • Kichaa cha mbwa kinasababishwa na Virusi, vimelea ambao ni wadogo kuliko bacteria.
  • Vimelea wa Kichaa cha mbwa wakiingia mwilini hushambulia na kuharibu mfumo kati wa fahamu
  • Mfumo kati wa ufahamu unajumuisha Ubongo na uti wa Mgongo.
  • Mfumo wa fahamu ulio na afya ni muhimu kwa; Kufikiri, Kuhisi, kuona, kupumua, kumeza, kula, kutembea na kuongea.

Wanyama gani wanapata kichaa cha mbwa?
Virusi vya kichaa cha mbwa vinaweza kumuingia mnyama yeyote aina ya mamalia.


  • Wanyama kama vyura, Ndege na Nyoka hawawezi kupata kichaa cha mbwa
  • Baadhi ya wanyama wanaoeneza kichaa cha mbwa ni, Mbwa, Popo, Mbweha na Paka
  • Mbwa ndiye kisababishi kikuu cha kichaa cha mbwa kwa Binadamu Duniani kote

Mnyama mwenye kichaa cha mbwa ana dalili gani?

  • Mbwa na paka wanapokuwa na kichaa cha mbwa huonyesha dalili kadhaa kama vile;
  • Kuwa na uoga na kuchanganyikiwa
Atataka kung’ata binadamu na wanyama wengine

  • “Kuogopa maji" na kushindwa kumeza kutokana na matatizo kwenye koo
  • Kudondokwa na mate kwa wingi
  • Wanyama wa mwitu wenye ugonjwa huu hubadili tabia zao kwa mfano, wanao onekana usiku peke yake huonekana wakizurura mchana.
  • Mbwa, paka, farasi, ng’ombe, kondoo na mbuzi pia huonyesha dalili za unyonge, kujiumiza au kujing’ata vile vile kutoweza kustahimili mwangaza.

Nifanye nini ili kuzuia kichaa cha mbwa?
  • Hakikisha wanyama wako wamechanjwa na afisa wa kudhibiti wanyama kuzuia kichaa cha mbwa
  • Ita wataalamu wa wanyama ukiona mnyama mgonjwa
  • Hakikisha kuwa sehemu za kutupia makombo na taka haziwavutii wanyama wa porini
  • Mnyama wa kufugwa atakiwa kuangaliwa kwa muda wa siku kumi(10) kwa dalili za kichaa cha mbwa.

Nifanye nini mnyama wangu anapomuuma mtu?


  • Mhimize mtu huyo akamwone daktari haraka iwezekanavyo.
  • Mwone daktari wako wa mifugo kubaini kama chanjo ya mnyama wako iko sawa kulingana na wakati wake.
  • Itabidi mnyama wako azuiliwe na aangaliwe kwa muda wa siku kumi (10) kwa dalili za kichaa cha mbwa.
  • Piga ripoti kwa afisa wako punde tu utakapoona dalili za ugonjwa wa kichaa cha mbwa.
  • Baada ya uchunguzi huu, hakikisha mnyama wako amepata chanjo dhidi ya kichaa cha mbwa.


Nifanye nini mnyama wangu anapoumwa?
  • Mwone daktari wako wa mifugo ili mnyama huyo apate chanjo dhidi ya kichaa cha mbwa hata kama alikuwa keshachanjwa.
  • Itabidi umzuilie mnyama wako na kumwangalia kwa muda wa siku arobaini na tano(45) ama zaidi kwa dalili za kichaa cha mbwa.
  • Mbwa na paka ambao hawakuwa na chanjo itabidii wauwawe au wazuliwe kwa muda wamiezi sita (6).
  • Wanyama wengine isipokuwa mbwa na paka, waking’atwa, itabidii wauwawe haraka iwezekanavyo

Nifanye nini ninapoumwa na mnyama?
  • Usiwe na hofu! Safisha kidonda vizuri kwa kutumia maji mengi na sabuni
  • Mwone daktari haraka iwezekanavyo kupata chanjo dhidi ya kichaa cha mbwa na ufuate maagizo yake.
  • Wasiliana na afisa wa kudhibiti wanyama kuthibitisha kama mnyama alikuwa amechanjwa.
  • Ikiwezekana, mzuilie ama mnase mnyama wa kufugwa ili aweze kuangaliwa kwa muda wa siku kumi(10) kwa dalili za kichaa cha mbwa.
  • Ikiwa ni mnyama wa pori, jaribu kumnasa ikiwezekana. La sivyo itabidi auwawe bila kuharibu sehemu ya ubongo kwani utahitajika kuchunguzwa kama alikuwa na kichaa cha mbwa.
  • Matibabu yanayofanyika kwa wakati mwafaka baada ya kuumwa yaweza kuzuia mtu kuambukizwa na kichaa cha mbwa.


Taarifa hii imeletwa kweni na;

KENYA WOMEN VETERINARY ASSOCIATION